TATIZO LA KUKOJOA KITANDANI (ENURESIS)

Tatizo la kukojoa kitandani kwa jina la kisayansi inaitwa enuresis ambapo mototo aliye katika umri ambao uwezo wa kuzuiya mkojo unataraji...


Tatizo la kukojoa kitandani kwa jina la kisayansi inaitwa enuresis ambapo mototo aliye katika umri ambao uwezo wa kuzuiya mkojo unatarajiwa; anakuabado anaendelea kukojoa kitandani au kwenye nguo.

ni tatizo la kushindwa kuzuia mkojo wakati wa mchana au usiku katika umri wa miaka mitano au zaidi.Watoto wengi wanaacha kukojoa kitandani usiku katika umri wa miaka mitatu. 

Asilimia 5 hadi 15 ya watoto wa miaka mitano wanaoendelia kijikojoa kitandani wengiwao ni wavulana ambayo ni asilimia 7 kuliko wasichana ambayo ni asilimia 3.Katika miaka 15 wanaoendelea kujikojoa kitandani ni asilimia 2 hadi 3 tu, na asilimia moja tu katika miaka 18. 

Kwahiyo kujikojolea siyo ugonjwa. Ni utofauki katika ukuaji wa fiziologia ya kuzuiya mkojo kwa mtoto.Mkojo unapo hifadhiwa katika kibofu cha mkojo, kibofu kinatanuka kama pulizo. Katika sehemu fulani neva za kutanua kuta za kibofu cha mkojo zinapeleka ishara ya kuzuia mkojo katika akili. Hii hutokea katika sehemu ya ubongo inayohusika na matendo yasiyo ya hiari. Kama ubongo wa motto haujapaya ishara hii, au ukishindwa kujua maana ya hiyo ishara, hatua ya makusudi ya kuzuia mkojo haitafanyika. 

Hii mara nyingi husababishwa na kuchelewa kwa ukuaji wa kibiologia wa utendakazi wa kuzuia mkojo.Ukuaji wa kijinsia inaweza kusababishwa na 

[1] kushindwa kwa akili kutambua ishara kutoka kwenye kibofu cha mkojo; 

[2] ujazo mdogo wa kibofu cha mkojo; au 

[3] usingizi nzito. Kwa sasa tafiti zinaonyesha kwamba watoto wanaokojoa kitandi ni wagumu kuamka kutoka usingizini kuliko ambao hawana tatizo hilo. Ni muhimu kutambua kwamba watoto hawajikojoei kwa makusudi na kawaida huona aibu kwa sababu hiyo.Wazazi wasiwadhalilishe kwa kuwaaibisha au kuwaadhibu.

Mara nyingi tatizo la kujikojolea imegawanyika katika sahemu mbili.ya kwanza ni pale mtoto anaposhindwa kukuza uwezo wa kuzuiya mkojo tangia utoto wake, ya pili ni pale mtoto anaweza kujizuiya kujikojolea kwa miezi sita au zaidi, halafu anaanza kujikojolea tena. Ya kwanza ni tatizo la kurithi na huwapata watu wa familia moja. Tafiti kutoka somo la vinasaba inaonyesha kwamba ikiwa wazazi wote walikuwa wanakojoa kitandani, asalimia 77 ya watoto watajikojolea zaidi ya miaka mitano na ikiwa mzazi mmoja alikuwa alikua na tatizo hili, asalimia 44 ya watoto watajikojolea zaidi ya miaka mitano. Na ikiwa wazazi wote hawakuwa na tatizo hili la kukojoa kitandani, asalimia 15 ya watoto watajikojolea zaidi ya miaka mitano.

CHANZO CHA TATIZO
Kuchelewa kukomaa kwa uwezo wa kibofu kuzuia mkojo ndio chanzo kikuu cha tatizo hili. Watoto hawa huwa hawana tatizo la hisia/kisaikolojia na kama wanalo ni matokeo tu ya maangalizi mabaya au matatizo wanayoyapata kutokana na tatizo walilonalo la kushindwa kuzuia mkojo kwa kukojoa kitandani au kujikojolea na sio kama chanzo kikuu.
Kwa upande mwingine,tatizo la kukojoa linalokuja baadae huweza kuwa limesababiswa na matatizo ya hisia au ya kisaikolojia na msongo wa mawazo(stress). Mara nyingi hii hutokea pale anapozaliwa mdogo wake, ugomvi wa wazazi, msongo anaoupata mtoto anapoanza shule au kutengana na wazazi. Matatizo kama haya na mengine yanayofanana yanaweza kumsababishia mtotto matatizo ya kihisia na kusababisha tatizo la kukojoa kitandani kuanza au kuzidi. Asilimia ndogo sana ya watoto wenye tatizo hili husababishwa na magonjwa au maambukizi katika sehemu ya kibofu au uwezo wa figo na hivyo kusababisha.
Tatizo hili limegawanyika katika sehemu mbili. 1. Tatizo la kukojoa kitandani wakati wa usiku (nocturnal enuresis) na lile la motto kujikojolea wakati wa mchana (diurnal enuresis). Tatizo la kukojoa kitandani wakati wa usiku huonekana zaidi kwa watoto wa kiume na lile la kujikojolea mchana mara nyingi huwa kwa wasichana.

MATIBABU NA JINSI YA KUMSAIDIA MTOTO
Ni muhimu kukumbuka kuwa watoto wenye tatizo hili wataacha kadiri wanavyokua na ikiwa utamsaidia inavyotakiwa, utamsaidia kuacha mapema zaidi.
Adhabu kali, kumpiga, au kumchapa motto mwenye tatizo hili humuongezea tatizo na kufanya tatizo lizidi au kuchelewa kuisha. Ni muhimu zana kutomuadhibu kumtisha au kumsema vibaya motto mwenye tatizo hili. Kufanya hivyo sio tu kama kutazidisha tatizo bali pia humfanya motto kuwa katika hatari ya kupata matatizo mengine ya kisaikolojia kwa wakati huo na hata baadae katika makuzi yake.
Ili kumsaidia motto mwenye tatizo hili ni muhimu na inashauriwa kumhakikishia na kumfariji motto kwa kumuonesha kua anapitia hatua ya kawaida ya makuzi na kuwa kadiri siku zinapita tatizo hilo linaisha. Hii itamsaidia motto kutopata msongo (stress) na kuusaidia mwili kufanya kazi yake vizuri ambayo hatimaye humsaidia kuondokana na tatizo hili mapema zaidi. Pia humzuia motto kuja kupata tatizo hili baada ya kuacha.
Pamoja na hayo; yafuatayo husaidia kumpa motto mafunzo na kuufundisha ubongo kutatua tatizo hili.

(1) kupunguza unywaji wa maji na ulaji wa vyakula vya majimaji kama vile uji masaa matatu kabla ya kulala.
(2) kumuamsha motto masaa mawili hadi matatu baada ya kulala ili akakojoe.
(3) kumpongeza siku ambazo hajajikojolea au kukojoa kitandani.
(4) Wazazi na ndugu (eg dada) kushirikiana na motto kujua mida ambayo tatizo la kukojoa linatokea na kisha kutumia nyenzo za kumuamsha nusu saa au lisaa kabla (mfano alarm) kufanya hivi kwa muda Fulani kutaufanya ubongo uweze kujifunza na motto atakua anaamka mwenyewe hata kabla ya kuamshwa au kabla ya alarm.

NOTE: Tafadhari usitumie dawa bila ushauri wa Daktari
3/recent/post-list
Name

Afya ya Kinywa na Meno,1,celebrities,1,crypto,2,Entertainment,8,icloud,1,Insurance,1,Investing,14,iphone,1,Kansa,7,luxury life,1,Magonjwa ya Zinaa,1,Magonjwa yanayoambukiza,1,maisha,2,Markets,2,NYT,286,Personal Finance,2,simulizi,1,sms,2,tech,1,Wanaume,9,wanawake,11,Watoto,5,
ltr
item
Business, Financial and Investment news and tools: TATIZO LA KUKOJOA KITANDANI (ENURESIS)
TATIZO LA KUKOJOA KITANDANI (ENURESIS)
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgV06_vBQOfhNRXNULu7UaAr6_Ntf4CLqgMN_5BafSRrvzQPsodgedzX3UmFhbNnXIVE0uSezLFUTKrQw06NDK3Ul5hLt9V0u5VCYZQCErbKC0SQf9Llhys06KRHBwWsiG12XvWP4O01Mer/s320/enuresis-infantil-1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgV06_vBQOfhNRXNULu7UaAr6_Ntf4CLqgMN_5BafSRrvzQPsodgedzX3UmFhbNnXIVE0uSezLFUTKrQw06NDK3Ul5hLt9V0u5VCYZQCErbKC0SQf9Llhys06KRHBwWsiG12XvWP4O01Mer/s72-c/enuresis-infantil-1.jpg
Business, Financial and Investment news and tools
https://www.wmgnews.com/2018/12/tatizo-la-kukojoa-kitandani-enuresis.html
https://www.wmgnews.com/
https://www.wmgnews.com/
https://www.wmgnews.com/2018/12/tatizo-la-kukojoa-kitandani-enuresis.html
true
7935609493103086404
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content